300. Mimi ni Mwana Kondoo
1. Mimi ni Mwana Kondoo
kikundini mwa Yesu,
ninafurahishwa sana
na Mchungaji wangu
mwema; anipenda kabisa,
anilisha vizuri.
2. Yeye akinilisha,
ninatunzwa vizuri
sina njaa, wala kiu,
sina shida, wala hofu,
ninaona raha tu
na furaha moyoni.
3. Heri yangu ni kubwa
nipendwaye na Yesu,
siku zangu zikiisha,
anipeleka mbinguni
anikumbatiapo
Yesu Mchungaji mwema.
Comments
Post a Comment