256. Njooni Tumsifu Mungu
1. Njooni tumsifuni Mungu
aliye Mwenyezi,
Mfalme wa popote
mbinguni na duniani.
Kwa sauti kuu
wote wamsifu Mungu,
kumpigia Mfalme shangwe.
2. Njooni tumsifuni Mungu
anayetawala,
vyote vizuri
akuongozaye na wewe.
Waruka juu
kama kwa nguvu ya tai,
ukiongozwa na Mungu.
3. Njooni tumsifuni Mungu
aliyetuumba
aliyetupa uzima
na wingi wa neema.
Shida nyingi
zimefukuzwa kwetu,
na Mungu mwenye rehema.
4. Njooni tumsifuni Mungu
aliyetulinda,
atubariki kwa pendo,
atupa riziki.
Ni Mwenyezi,
atutendea makuu,
anatupenda kwa kweli.
5. Njooni tumsifuni Mungu,
tumsifu kwa nyimbo,
kama Daudi imbeni
na mashangilio.
Tusisahau ndiye nuru ya roho.
Tumsifu hata milele.
Comments
Post a Comment