268. Msingi wa Kanisa

1.  Msingi wa Kanisa 

    ndiye Yesu Bwana; 

    kiumbe kipya chake, 

    alipenda sana; kutaka litafuta 

    alishuka chini, naye kwa kuja

    kwake akafa mtini.


2.  Lina kila taifa, kisha ndilo moja,

    wokovu wake una 

    Mwokozi mmoja; 

    Uzazi ni mmoja, na moja imani,

    chakula ni kimoja, moja tumaini.

 

3.  Watu hustaajabu 

    kwa mashaka mengi 

    yawapatayo nje hata ndani pia.

    Ila watakatifu huomba,

    wakesha usiku ni kilio,

    asubuhi raha.


4.  Mashaka na taabu 

    hata vita vyake,

    vyangoja matimizo 

    ya amani yake,

    ndipo kwa macho yetu 

    tuone utukufu

    Kanisa lishindalo litastarehe juu. 

Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu