316. Ati Tuonane Mtoni?
1. Ati tuonane mtoni?
Maji mazuri ya mbingu;
Yanatokea mwangani,
penye kiti cha Mungu.
Naam, tuonane mtoni!
Watakatifu,
kwenu ni mtoni!
Tutakutanika mtoni
penye kiti cha Mungu.
2. Tukitembea mtoni
na Yesu Mchunga wetu
daima tu ibadani
usoni pake kwetu.
Naam, tuonane …
3. Kwang’ara sana mtoni,
cha Mwokozi ni kioo,
milele hatuachani
tumsifu kwa nyimbo.
Naam, tuonane …
4. Si mbali sana mtoni
karibu tutawasili,
mara huwa furahani
na amani ya kweli.
Naam, tuonane …
Comments
Post a Comment