251. Moyo Wangu Furahiwa

1.  Moyo wangu furahiwa, 

    tazama neema ya Bwana

    katika mwaka huu. 

    Tazama mashamba yote

    yanavyostawi vizuri, 

    yakupendeza wewe,

    yakupendeza wewe.


2.  Miti yote yachipuka 

    Yote yatoa maua 

    yanayong’aa vizuri.

    Milima hata mabonde 

    tena nyika zimepambwa 

    kupita nguo zote,

    kupita nguo zote.


3.  Chore alia hewani, 

    vichakani kurumbiza

    porini ni kulungu.

    Pote sauti za wanyama,

    Muumbaji azisikia 

    sifa za hivi vyote,

    sifa za hivi vyote.


4.  Mwenyezi Mungu bariki 

    vyote ulivyoviweka 

    chini ya mbingu yako.

    Na mioyo yetu ing’ae 

    kwa neema yako nzuri mno

    uliyotupa wewe, 

    uliyotupa wewe.


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu