271. Baba Yetu Uliye Mbinguni
1. K: Baba yetu uliye mbinguni,
W: Jina lako litukuzwe
K: Ufalme wako uje
mapenzi yatimizwe
W: Jina lako litukuzwe.
2. K: Hapa duniani
kama mbinguni,
W: Jina lako litukuzwe.
K: Utupe leo hii riziki yetu.
W: Jina lako litukuzwe
3. K: Utusamehe Baba,
makosa yetu,
W: Jina lako litukuzwe.
K: Kwa jinsi sisi nasi
tunavyosamehe.
W: Jina lako litukuzwe.
4. K: Usitutie kamwe
majaribuni
W: Jina lako litukuzwe.
K: Bali utuokoe katika
uovu
W: Jina lako litukuzwe.
5. K: Kwa kuwa wako
ufalme, mamlaka yote.
W: Jina lako litukuzwe.
K: Na utukufu sasa
na hata milele.
W: Jina lako litukuzwe.
6. K: Amin, Amin,
tunakushukuru.
W: Jina lako litukuzwe.
K: Uhimidiwe Bwana
wee Mfalme wetu.
W: Jina lako litukuzwe
Comments
Post a Comment