306. Yesu Hukaribisha
1. Yesu hukaribisha
wenye mabaya! Pasheni
wote waliokosa
Neno hili la faraja,
walisikie vema:
“Yesu ndiye Mwokozi.”
2. Twastahili kufa tu,
Yesu hutuhurumia, akatufungulia
mlango wa rehema kubwa.
Nasi sasa twajua:
“Yesu ndiye Mwokozi.”
3. Akipotea kondoo,
Mchunga mwema amtafuta.
Yesu Mchunga wa watu
anawatafuta wote
waliokosa njia:
“Yesu ndiye Mwokozi.”
4. Yesu hukaribisha
wakosaji, hata mimi
ameniita kwake,
mbingu imefunguliwa.
Naungama nikifa:
“Yesu ndiye Mwokozi.”
Comments
Post a Comment