294. Mtumwa wa Yesu Huona
1. Mtumwa wa Yesu huona
furaha nyingi mno.
Si mtumwa wa unyang’anyi,
ni mtoto wa Mungu.
2. Mtumwa wa dhambi haoni
njia ya wokovu.
Mtumwa wa Yesu hakosi
njia ya mbinguni.
3. Mpenda makosa huona
ugomvi na shida.
Watu wa Yesu huona
upendo na raha.
4. Ubaya wapata kufa,
ni mshahara wake.
Yesu atuokoaye
aleta uzima.
5. Bwana, umenikomboa
nami nakupenda,
nakutumikia wewe
simtaki mwingine.
6. Nakuomba Bwana Yesu,
unipeleke juu;
ulipo ndipo pazuri
pa mtumishi wako.
Comments
Post a Comment