282. Mimi Mkosaji Nakuomba
1. Mimi mkosaji nakuomba
Mungu wangu Mtakatifu:
Uniendee kwa upole,
nisipotee kabisa.
Uliye na huruma kuu,
Mungu, unihurumie!
2. Naona hofu kubwa sana
kwa ajili ya makosa.
Nisaidie kwa rehema,
niliye mwenye ubaya.
Uliye na huruma …
3. Unisikie Baba yangu,
nikikulilia sasa.
Yaondoe makosa yangu,
moyo upate kupoa.
Uliye na huruma …
4. Usinitupe kwa ukali
kama nilivyostahili.
Unikubali tena, Baba,
katika kundi la wana.
Uliye na huruma …
5. Ni neno hili liwezalo
kunipa tena moyo mkuu;
“Makosa yameondolewa
Nawe usikose tena”
Uliye na huruma …
6. Najua umenisikia,
sioni shaka moyoni.
Sababu hii ninamaliza
kuomba kwangu kwa moyo.
Uliye na huruma …
Comments
Post a Comment