302. Mungu Wetu Ndiye Boma
1. Mungu wetu ndiye boma,
silaha tena ngao,
atukingiaye shida
zitushikazo sisi.
Adui wa kale
afanya hila ya kutushinda,
ni mwenye nguvu kuu,
hakuna amwezaye.
2. Nguvu zetu hazifai
tunashindwa upesi.
Lakini tunaye shujaa
aliye mwenye nguvu.
Jina lake nani?
Ni Yesu Kristo
Mungu mwenyewe,
hapana mwingine
ni mshindaji wa wote.
3. Shetani akikusanya
majeshi yake yote.
Hatuogopi kabisa
kwani tutawashinda!
Mfalme wa dunia akunja uso
ana hasira, lakini ni bure:
Neno moja tu lamweza!
4. Neno la Mungu lashinda!
Halitafuti msaada.
Mungu yu pamoja nasi na roho
ya hekima. Wakitunyang’anya
watoto wenzi;
mwili na mali haidhuru!
Si kitu!
Twamshika Yesu Mfalme.
Comments
Post a Comment