274. Ewe Bwana Ndiwe Mchunga
1. Ewe Bwana ndiwe
Mchunga wangu mwema.
Sitapungukiwa na kitu,
kwani u pamoja nami.
2. Wanilaza kwenye
malisho tele;
Wanitangulia vizuri,
kwani wanipenda sana.
3. Nafsi yangu
imehuishwa nawe,
na kuongozwa kwa haki,
kwa ajili ya Jina lako.
4. Nikipita hata
bonde la mauti,
sitayaogopa mabaya,
kwani Wee u gongo langu.
5. Umeandaa meza
mbele yangu mimi,
ili na watesi waone,
kwamba ndiwe mwenye neema.
6. Kichwa changu
kimepakwa na mafuta,
Kombe langu linafurika;
Haya umefanya yote.
7. Wema wako
umenifuata hasa.
Nami nitaishi na wewe,
kwako, Bwana siku zote.
Comments
Post a Comment