324. Haya! Usiku Waja

1. Haya! Usiku waja, 

   fanya bidii nyingi, 

   Amka mapema sana, 

   usichelewe!

   Fanya kaziyo mchana 

   anza asubuhi!

   Haya!  Usiku waja, 

   mwisho wa kazi.


2. Haya! Usiku waja, 

   jua laenda juu.

   Umtumikie Yesu 

   kwa nguvu zote.

   Usiogope jasho,

   kazi hii ni bora. 

   Haya! Usiku waja, 

   mwisho wa kazi.


3. Haya! Usiku waja,

   shinda mchana kutwa!

   Fanya bidii jioni,

   jua likichwa.

   Kazi ya Bwana Yesu

   haina kuchoka. 

   Haya! Usiku waja, 

   mwisho wa kazi. 

 

Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu