339. Ee Ndugu, Twendeni Kazini

1. Ee ndugu, twendeni 

   kazini kwa Bwana, 

   tufuate nyayo 

   za Bwana, mwenyewe; 

   kwa nguvu ya Roho 

   atiaye upya, 

   tupate upendo 

   wake wa ajabu.

         Mfalme mkuu yuko juu 

         Ye shujaa siku hii

         katika kazi hii 

         thawabu ni taji 

         atakapokuja mfalme. 


2. Tukikesha sana, 

   tukimwomba Bwana 

   Yeye atatupa yale tuombayo.

   Tuwe mashahidi: 

   “Aondoa dhambi, 

   aosha mioyo ya watu wajutao.” 

         Mfalme mkuu …


3. Tuwatafuteni watu wapotevu, 

   na tuwatulize watu wa huzuni 

   tuwatunze watu walio maskini:

   tuwe nuru gizani, tuwaangaze.

          Mfalme mkuu … 


4. Tukimshambulia

   yule mwovu mkubwa, 

   tumheshimu sana 

   Bwana Mungu wetu. 

   Kazi yetu ni hii!

   Ee jamaa Twendeni! 

   Tukishinda, Bwana 

   atatupa tuzo.

           Mfalme mkuu … 


5. Tushangilieni 

   kwa nyimbo za shangwe,

   tusifu uzuri ule wa mbinguni.

   Siku ile Bwana akija atupa 

   taji la uzima,  thawabu ya vita.

             Mfalme mkuu …


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu