338. Mawimbi Yanavuma

1. Mawimbi yanavuma,

   yachafuka sana.

   Na wokovu hapana, 

   pwani hatuoni!

   Giza liko popote,

   Mmoja ndiye Mwokozi; 

   Bwana Yesu,  tuokoe Bwana.


2. Mwezi ukichelewa, 

   nyota zikienda,

   chombo kikivunjika,

   Mwokozi ni nani?

   Mwokozi ndiye Bwana,

   Yeye nahodha wetu. 

   Bwana Yesu,  tuokoe Bwana.


3. Mawimbi yatulia

   kukiwa shwari kuu. 

   Wewe Muumbaji wetu 

   tunakushukuru; 

   twakuimbia Bwana,

   leo na siku zote. 

   Bwana Yesu,  tuokoe Bwana.


4. Shida za kufa kwangu 

   zinaponijia 

   Bwana uniokoe 

   nisizame mimi.

   Unipe mkono wako 

   Wewe unipendaye. 

   Bwana Yesu,  tuokoe Bwana.


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu