337. Wakristo Ifuateni
1. Wakristo ifuateni
vita yake Mungu.
Wote wachaguliwao
ondokeni hima.
Haya bendera juu
nyote fuateni!
Baragumu zinalia!
Njooni, njooni nyote!
2. Askari wote waseme:
“Mungu yuko kwetu.”
Mwokozi Yesu mwenyewe
atupigania.
Wote na malaika watusaidia.
Pamoja na Shujaa wetu
twamshinda adui.
3. Kavumilieni taabu,
askari wa Yesu! Ikingieni mioyo
mishale ya mwovu.
Haya, yaacheni
mambo mapotovu.
Mfanya vita afikiri
mambo ya vita tu.
4. Shikeni silaha zote
za vita kali hii.
Upanga ulio mkali
ni Neno la Mungu.
Lenu tegemeo liwe ngao yenu.
Ukanda wa viunoni
ni kweli na haki.
5. Piganeni kwa kishujaa
kila siku vema.
Na Yesu awafundishe
mambo ya vita hii.
Ngoja, watashinda
wao wenye bidii.
Taji yenu ni tayari;
Uzima wa mbingu.
Comments
Post a Comment