336. Tumfuate Bwana Yesu
1. Tumfuate Bwana Yesu,
kiongozi ni Yeye;
atuonyeshaye njia
ya kushinda dunia.
Tukikaa ulimwenguni
twende njia ya mbingu,
tupendane vizuri,
tuamini kwa mioyo.
Yesu tutangulie
nasi twakufuata.
2. Tumfuate Bwana Yesu,
hata tukiteseka.
Hapa pana shida nyingi,
huko iko furaha.
Wapandao kwa machozi
watavuna kwa shangwe.
Mungu atabadili
kulia kuwe kucheka.
Tulipoteswa hapa
tutaona furaha.
3. Tumfuate Bwana Yesu,
tufe pamoja naye.
Kufa kwake kwatuponya
katika upotevu.
Duniani tuishinde
miili yetu na tamaa;
Yesu atufufua
miili yetu kaburini.
Yesu nitakufia,
nikuone milele.
4. Tumfuate Bwana Yesu,
kwani amefufuka.
Tena atawafufua
watu siku ya mwisho.
Sisi tu viungo vyake,
tutafika huko juu
enzini mwa mkuu wetu
aliyetuita kwake.
Yesu nakupa moyo,
nipe uzima wako.
Comments
Post a Comment