335. Sisi Tulio Watoto

1. Sisi tulio watoto

   wa Mwenyezi milele. 

   Tupendane kama Yesu 

   alivyotufundisha.

   Yote tunayotaka 

   watu watufanyie

   na sisi tuwafanyie,

   ndiyo amri ya Mwokozi.


2. Tutumikiane vema 

   kwa upendo wa nguvu.

   Hivi tunazaa matunda

   yampendezayo Mungu. 

   Tumsaidie ndugu

   kwa hiari shidani, 

   tukumbuke hata sisi 

   twapewa vyote na Mungu.


3. Tusiwachukie ndugu 

   waliotukosea;

   ila tupatane tena 

   tukisameheana.

   Mwenye dhambi tumwonye

   kwa upole na upendo: 

   hivi tutamsaidia, 

   asikose njia nzuri.


4. Tusiwahukumu ndugu 

   waliokosa sana. 

   Tukumbuke, hata sisi 

   tuna makosa mengi.

   Tumsikie Mwokozi 

   akionya Wakristo;

   Usimhukumu mwenzio, 

   ili usihukumiwe.

 

5. Bwana utuvike sote 

   mavazi ya uongofu.

   Ututengeneze vema tule

   karamu kwako

   Mwisho uniambie;

   Ewe mtumwa mwema 

   njoo  ulikuwa mwaminifu, 

   nakupa furaha zangu.


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu