334. Nyota Yenye Nuru
1. Nyota yenye nuru,
mwamba wa nguvu,
kiongozi wangu,
fimbo mkononi,
mkate wa uzima,
chemchem ya neema,
/: Tumaini langu
ndiwe Bwanangu. :/
2. Nisipokushika nguvu i wapi?
Nani aondoa
mzigo wangu mkuu?
Nisipokushika sina amani,
/: sina tumaini,
sina upendo. :/
3. Nitakufuata ulimwenguni
Mpaka nifikapo
kwako mbinguni.
Kule nitaanza tena kusifu,
/: Nitakuimbia
Wewe Bwanangu. :/
Comments
Post a Comment