333. Njooni kwa Mponya
1. Njooni kwa Mponya,
njooni leo,
sikilizeni Neno lake.
Anapenda kutubariki,
atuita: “Njooni!”
Kweli tutaona furaha
tukifika kwenye raha kuu,
tukisafishwa mioyo yetu
na Yesu Mwokozi.
2. Njooni kwa Yesu, mfuateni,
mpeni mioyo itikeni!
Kweli ni boma likingalo
hatari zozote.
Kweli tutaona …
3. Amini, Bwana awapenda.
Amini, atawabariki,
atawahurumia wote,
wamjiao yeye.
Kweli tutaona …
Comments
Post a Comment