332. Njia Ile Nyembamba
1. Njia ile nyembamba
iendayo uzimani!
Heri anayekwenda
njia hii na Bwana Yesu.
Kaza mwendo ufike,
usichoke njiani.
2. Heri waliokuwa
waaminifu hata kufa,
walioshinda tamaa
wanaomfuata Yesu,
watapewa mshahara,
taji ya washindao.
3. Yesu ametufia
msalabani kwa uchungu,
akapaa mbinguni juu
akapata utukufu.
Tutapewa uzima
tukimfuata Yesu.
4. Ndugu tusiogope
njia yenye shida nyingi.
Kesheni muombeni
Bwana atutegemeze.
Tutaweza kushinda
tukimshika Yesu tu.
Comments
Post a Comment