331. Nivute Kwako Bwana Yesu
1. Nivute kwako, Bwana Yesu,
katika shida hata furaha,
unipokee kwa rehema,
/: niangalie,
ee Bwana wangu.:/
2. Nivute kwako! Sina kitu
ninachoweza kukutolea,
ila moyo huu wenye dhambi.
/: Yesu Mwokozi
unisafishe.:/
3. Nivute kwako! Nitaacha
yote yazuiayo baraka.
Nakutolea, Bwana wangu.
/: mali na furaha
za dunia.:/
4. Nivute kwako! Mpaka mwisho
vita na hatari zikiisha.
Mpaka nifanane na Wewe,
/: Wewe, ee Yesu,
furaha yangu!:/
Comments
Post a Comment