330. Tunakwenda Mbinguni
1. Tunakwenda mbinguni!
Duniani twasafiri
wenye taabu nyingi,
mpaka tufike mbinguni.
Hapa tu wapitaji,
kule sisi wenyeji.
2. Ninakwenda mbinguni!
Roho yangu; angalia
mambo yaliyo ya juu;
usishikwe na dunia.
Roho iliyong’azwa,
na Mungu yampendeza.
3. Ninakwenda mbinguni,
ndivyo ninavyoambiwa.
Hili lanionyesha
raha na furaha zote,
nitakazozipata
nikifika mbinguni.
4. Ninakwenda mbinguni
kufa kutanipeleka
pale nitakapokaa,
shida zikiisha zote.
Namfuata Mwokozi
aliyetangulia.
5. Ninakwenda mbinguni
nitashika neno hili.
Nitashinda kabisa
majaribu hata taabu,
nikikumbuka hivi:
ninakwenda mbinguni!
Comments
Post a Comment