328. Ndugu, Kundi Lake Mungu

1.  Ndugu, kundi lake Mungu 

    atupendaye sana,

    tumfuate Mponya wetu

    tukipendana vema. 

    Yeye kichwa, tu viungo, 

    Yeye nuru yetu kuu;

    Yeye Bwana, sisi ndugu.

    Atupenda, twampenda.

 

2.  Njooni watoto wa Mungu,

    sasa turudi kwake,

    tumwapie: Sisi sote 

    twataka kukushika.

    Na upendo wa kindugu 

    utakapolegea, 

    tutamsihi Bwana wetu 

    azidishe upendo.


3.  Enyi viungo vya Yesu,

    pendaneni kwa bidii, 

    kazeni kujipa mioyo 

    ya kuwafia ndugu.

    Kama alivyotupenda 

    Yesu akatufia.

    Nasi tusipopendana 

    ahuzunika sana.

 

4. Yesu uwaunganishe 

   watu wakupendao,

   Wapendane kwa mioyo,

   kama unavyotaka. 

   Watumikiane vema 

   na kufurahishana;

   wawe wote kundi moja 

   na Wewe Mchunga wao. 

Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu