327. Mwokozi Yesu Asema
1. Mwokozi Yesu asema:
Nifuateni nyote!
Acheni ulimwengu huu,
utafuteni kwanza
ufalme wa mbinguni tu
na haki yake kwa bidii.
2. Ninaing’aza mioyo,
iweze kwenda sawa,
atakayenifuata,
haendi kwenye giza.
Natangulia Wakristo
washike njia ya kweli.
3. Unyenyekevu na pendo,
zajaa moyoni mwangu,
na kinywa changu kimejaa,
maneno ya upole.
Nami namngojea Mungu
kwa haja zote za roho.
4. Naonyesha yanayofaa;
yafuateni vema
Itakaseni mioyo
isiwe na uchafu.
Nalinda roho za watu,
wafike kwangu mbinguni.
5. Atakaye kuiponya
nafsi, huipoteza;
aipotezaye nafsi
atafika kwa Mungu.
Asiyeuvumilia
msalaba hanistahili.
6. Sababu hii tumfuate
Bwana kwa nguvu zote.
Tuvumilie mateso
kwa ajili ya Yesu.
Asiyeshindana vema
hapewi taji ya mbingu.
Comments
Post a Comment