326. Mbona Wasumbukia

1.  Mbona wasumbukia

    mambo ya ulimwenguni, 

    yaliwayo upesi,

    yafananayo na taka.

        Umtafute Yesu tu,

        ukitaka furaha. 


2.  Zoeza roho yako 

    kufikiri mambo mema, 

    yaliyo ya mbinguni

    na rehema yake Mungu. 

         Umtafute Yesu tu … 


3.  Mara nyingi wataka 

    kupumzisha moyo wako. 

    Iko chemchemi ya neema,

    utakapopata raha.  

          Umtafute Yesu tu …


4. Ukimbie hatari 

   za ufalme wenye giza:

   umchague Mwokozi 

   afurahishaye moyo. 

         Umtafute Yesu tu …


5.  Kweli ulimwengu huu 

    unapenda mambo mengi 

    yasiyokupendeza 

    Yesu uliyetuita. 

          Umtafute Yesu tu …


6.  Umezaliwa tena

    kwa maji na Roho wake. 

    Basi usifuate

    mambo ya mtu wa kale. 

         Umtafute Yesu tu …


7.  Ukumbuke kwa bidii 

    utukufu wake Mungu,

    inua moyo wako,

    kwa kuomba na kusihi. 

         Umtafute Yesu tu …


8. Ukifanya hivi tu

   hutakosa mwisho mwema,

   Yesu akupendaye 

   atakupa utukufu. 

         Umtafute Yesu tu …


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu