325. Mahali ni Pazuri
1. Mahali ni pazuri
ndugu wanapokaa,
/: wakipatana vema
na wakipendana.:/
2. Kama umande mzuri
unyweshavyo shamba,
/: hivyo na Mungu wetu
abariki ndugu.:/
3. Upendano hujenga
boma zuri kwao,
/: wakae na amani
waliookoka.:/
4. Na ulimwengu wote
wavutwa nuruni,
/: halafu kundi moja na
Mchunga mmoja tu.:/
Comments
Post a Comment