323. Bwana Utusaidie

1. Bwana utusaidie

   tuwe wanafunzi wako wazuri.

   Utung’aze macho yetu,

   utupe sote mioyo myeupe.

   Tufuate njia zako, 

   tuwe wenye nia moja.

   Twakuomba:

   Uzidishe Nguvu kwetu.


2. Wote waona furaha, 

   wampendao 

   Bwana Yesu kwa moyo.

   Nasi tuwe watu wake, 

   tuwe kama 

   shamba zuri la Yesu.

   Anapenda kuingia 

   na kukaa mioyoni mwetu.

   Umpokee ukitaka kuokoka.


3. Sikia kuomba kwetu 

   Yesu upendaye kutubariki,

   Uzidi kutubariki, tusishindwe,

   shida zikitujia. 

   Uongoze watu wako, 

   tufuate njia zako.

   Mpaka tutakapoingia mbinguni.


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu