322. Mjini Kwake Babangu
1. Mjini kwake Babangu
ndipo pa raha
tutafika juu kwake
tukae naye.
Kuna raha, Kuna raha.
/:Kwake Bwana kuna raha:/
Lini tutafika kwake
tuungane na malaika
mjini kwake, mjini kwake.
2. Pale kwake Babangu
ndipo pazuri.
Siku ile kuu mno
ya kupaona.
Kuna raha. Kuna raha.
/:Kwake Bwana kuna raha:/
Mji ung’arao mno
ni makao ya malaika
mjini kwake, mjini kwake.
3. Nikipanda mlimani
na kuyaona
yote ya utukufu aliyofanya.
Kuna raha. Kuna raha.
/:Kwake Bwana kuna raha:/
Yote yanisimulia
ufahari wake Baba
mjini kwake, mjini kwake.
4. Njoo mwenzangu tazama
yote ya Mungu
yote ameyafanya kwa ajili yetu.
Kuna raha. Kuna raha.
/:Kwake Bwana kuna raha:/
Tuinue macho yetu
tumtazame Mwumba wetu
mjini kwake, mjini kwake.
Comments
Post a Comment