320. Yesu Nakupenda, u Mali Yangu

1. Yesu nakupenda, u mali yangu,

   anasa za dhambi sitaki kwangu

   na Mwokozi aliyeniokoa, 

   sasa nakupenda, kuzidi pia.


2. Moyo umejaa mapenzi tele 

   kwa vile ulivyonipenda mbele

   uhai wako ukanitolea

   sasa nakupenda, kuzidi pia.


3. Ulipoangikwa msalabani

   tusamehewe tulio dhambini;

   Taji ya miiba uliyoivaa

   sasa nakupenda, kuzidi pia.


4. Niwapo hai, niwapo maiti, 

   kupendana nawe kamwe siachi,

   hari za kifo zikinienea,

   sasa nakupenda, kuzidi pia.


5. Mawanda mazuri hata  maskani

   niyatazamapo huko mbinguni.

   Tasema na taji nitakalovaa 

   sasa nakupenda, kuzidi pia.


Comments

Popular posts from this blog

276. Nina Haja Nawe

257. Haya ee Moyo Wangu

265. Mganga Wetu ni Karibu